IQNA

Wanaharakati wa nchi 20 wataka Sheikh Nimr aachiliwe huru

19:19 - August 02, 2015
Habari ID: 3338080
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameandamana katika nchi 20 duniani wakitaka Saudi Arabia imuachilie huru msomi wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia Sheikh Nimr al-Nimr.

Kwa mujibu wa gazeti la al-Akhbar, waandamanaji hao wametangaza kufungamana kwao na msomi huyo wa Kiislamu anayeshikiliwa katika jela za kuogofya za ufalme wa Saudia.
Maandamano hayo yamefanyika katika nchi kama vile Colombia, Switzerland, Marekani, Ujerumani, Iran, Bahrain, New Zealand, Canada, Ufaransa, Ghana na Lebanon.
Sheikh Nimr alitiwa korokoroni mwezi Julai mwaka 2012 kufuatia maandamano ya wananchi katika eneo la Qatif nchini Saudi Arabia.
Anatuhumiwa kuwa alitoa hotuba zilizo dhidi ya utawala wa kifalme na kuwatetea wafungwa wa kisiasa. Kukamatwa Sheikh Nimr kuliibua machafuko makubwa katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Mwezi Machi mwaka huu mahakama ya rufaa ya Saudia iliidhinisha hukumu ya kifo dhidi ya mwanazuoni huyo wa Kiislamu lakini hukumu hiyo ya kidhalimu bado haijatekelezwa.../mh

3337383

captcha