IQNA

Misri yawafunga wafuasi 452 wa Ikhwanul Muslimin

12:33 - August 13, 2015
Habari ID: 3341805
Wafuasi 452 wa Harakati ya Ikwanul Muslimin nchini Misri wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu hadi 25 jela katika hukumu iliyotolewa na mahakama ya kijeshi.

Wanachama hao wa Ikhwanul Muslimin wametuhumiwa kushiriki kwenye vurugu za kupinga serikali kufuatia kupinduliwa Rais Mohamed Morsi mwaka 2013.  Baadhi ya waliohukumiwa na mahakama hiyo ya kijeshi mjini Alexandria Jumanne ni kiongozi mwandamizi wa Ikhwanul Muslimin Gamal Heshmat ambaye yuko uhamishoni nchini Uturuki. Katiba mpya ya Misri inaruhusu mahakama ya kijeshi kutoa hukumu kwa raia wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu dhidi ya idara za jeshi au zilizo chini ya usimamizi wa jeshi.

Mursi alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya demokrasia Misri na baada ya kuwa madarakani kwa mwaka mmoja, aliondolewa madarakani mwezi Juni mwaka 2013 katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na mkuu wa jeshi wakati huo Abdul Fattah el Sisi ambaye sasa ni rais wa nchi hiyo.../mh

3341616

Kishikizo: misri ikhwan mursi
captcha