IQNA

Mahathir Mohammad

Masuni Malaysia wawakubali Mashia kama Waislamu wenzao

14:56 - September 15, 2015
Habari ID: 3362892
Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Mahathir Mohammad ametoa wito kwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni waliowengi Malaysia kuwakibali Mashia kama Waislamu wenzao ili kzuia mapigano ya madhehebu nchini humo kama yale yanayoshuhudiwa katika baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati.

Katika hotuba Jumatatu Usiku katika kikao kilichofanyika mji wa Shah Alam nchini Malaysia, Mahathir amewakumbusha hadhirina kuhusu itikadi ya Kiislamu kuwa mtu huwa Mwislamu pale anapotamka Shahada ya La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah yaani Hakuna Apasaye kuabudiwa ila Allah na Mohammad ni Mtume Wake.
Ameongeza kuwa Masuni na Mashia wote wanatamka shahada hizo mbili.
Mahathir amesema Wamalaysia wamekuwa wakiishi pasina kuwepo malumbano ya kimadhehebu na kwamba aghalabu ni Masuni wa madhehebu ya Shafii na kwamba kwamba pia kuna idadi chache ya Mashia.
Amesema Malaysia ingali inashuhudia amani ikilinganishwa na baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati na hivyo ametoa wito wa kudumishwa amani kupitia kustahimiliana  watu wenye mitazamo tafauti. Akiashiria Waislamu wa madhehebu ya Shia amesema: "Hatuna haki ya kusema si Waislamu kwa sababu tu hawako kama sisi."
Mahathir amegusia pia mapigano baina ya Mashia na Masuni katika baadhi ya nchi za Kiislamu na kusema wanaojihusisha na mapigano ya kimadhehebu wanatekeleza malengo ya Mayahudi na Wamarekani.
Ameongeza kuwa: "Mayahudi na Wamarekani sasa wanatucheka." Waziri mkuu wa zamani wa Malaysia amebainisha kuwa kwa kujihusisha na malumbano ya kimadhehebu, Waislamu wanawahudumia maadui huku akisisitiza umuhimu wa kuangazia zaidi nukta za pamoja kuliko nukta za kutenganisha ambazo ni chache.../mh

3362727

captcha