Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani (CAIR) limetoa taarifa na kusema kundi la watu wenye misimamo mikali ya chuki dhidi ya Uislamu na ambao hutumia mabavu wanapanga kuandaa maandamano nje ya misikiti kote Marekani mnamo Oktoba 10. Waandalizi wa maandamano hayo wamesema watatumia silaha katika majimbo ya Marekani, na kwa msingi huo yamkini ghasia zikaibuka.
CAIR imesema maandamano hayo dhidi ya Uislamu yanakuja katika hali ambayo kumeshuhudiwa ongezeko la jinai zinazohusiana na chuki za kidini huku Uislamu na Waislamu wakilengwa na watu wenye msimamo mikali.
Kwa ujumla Waislamu Marekani wametakiwa kuchukua tahadhari katika maeneo yote ya umma na hata majumbani mwao huku wakijuliana hali na kuwasaidia wale ambao yamkini wakadhuriwa katika siku hiyo.