IQNA – Mwanamke wawili Waislamu nchini Marekani wamewasilisha kesi dhidi ya Kaunti ya Orange na idara yake ya sheriff, wakidai kuwa maafisa walilazimisha kuondolewa kwa hijabu zao wakati wa kuwatia mbaroni katika maandamano ya mwaka 2024 huko UC Irvine.
Habari ID: 3480883 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/02
IQNA – Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR) limemtaja mbunge katika Bunge la Marekani Randy Fine (R-FL) kuwa “mwenye msimamo mkali wa chuki dhidi ya Waislamu”, likimjumuisha katika orodha yake ya watu wenye chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia), kutokana na kile ilichokiita rekodi ya muda mrefu ya matamshi ya uchochezi dhidi ya Waislamu na Wapalestina.
Habari ID: 3480821 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/11
IQNA – Serikali ya Ufaransa imeshutumiwa kwa kulenga shirika la Ulaya linalojitolea kupambana na chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3480767 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/31
IQNA – Waislamu wanaosimamia mradi wa ujenzi wa mtaa wao mpya huko Texas, Marekani wamesema uchunguzi wa serikali na shirikisho una dosari.
Habari ID: 3480665 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/10
IQNA – Mmarekani mwenye asili ya Kiarabu amefungua kesi ya ubaguzi dhidi ya Shirika la Big Jay’s Auto Sales huko Shelby Township, Michigan, Marekani akidai kwamba mfanyakazi wa shirika hilo alitoa matamshi ya udhalilishaji kuhusu imani yake ya Uislamu wakati wa mazungumzo ya uuzaji wa gari.
Habari ID: 3480592 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/25
IQNA- Sheria mpya imetangaza Idul Adha na Idul Fitr kuwa sikukuu rasmi katika jimbo la Washington nchini Marekani.
Habari ID: 3480522 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/11
IQNA – Wazazi na walimu nchini Marekani wametakiwa kuhudhuria webinari (warsha za mtandaoni) mbili zijazo zinazolenga kuunga mkono wanafunzi Waislamu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3480210 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/13
Waislamu Marekani
IQNA – Mji wa Michiganu Januari kuwa "Mwezi wa Urithi wa Waislamu wa Marekani," ili kutambua michango muhimu ya Waislamu wa Marekani katika utamaduni, uchumi, na jamii katika jimbo hilo.
Habari ID: 3480036 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/11
IQNA - Kuna mashirika mengi ya kutoa misaada ya Kiislamu nchini Marekani yanayojaribu kupeleka misaada Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wanaokumbwa na vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na Israel, lakini wanakabiliwa na vikwazo na ubaguzi mbalimbali.
Habari ID: 3479828 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/30
Waislamu Marekani
IQNA - Kundi la kutetea haki za Waislamu Marekani limelitaka Baraza la Seneti kumkataa Peter Hegseth, mteule wa Donald Trump kuwa Waziri wa Ulinzi (Pentagon), kutokana na misimamo yake dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3479761 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/16
IQNA - Kundi la kutetea haki za Waislamu Marekani limemkosoa Rais wa Marekani Joe Biden "kushiriki kikamilifu katikaa uhalifu wa (Israeli) dhidi ya ubinadamu".
Habari ID: 3479692 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/03
Waislamu Marekani
IQNA - Kundi la kutetea haki za Waislamu nchini Marekani limemsuta rais wa zamani Bill Clinton kwa jaribio lake la kuutetea utawala katili wa Israel ambao unaendesha mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
Habari ID: 3479678 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/11/01
Chuki dhidi ya Waislamu
IQNA - Shambulio dhidi ya mwanamke aliyevaa keffiyeh (skafu ya kichwa ya Wapalestina) huko Brooklyn limelaaniwa huku kukitolewa wito wa mashtaka ya uhalifu wa chuki kwa wausika.
Habari ID: 3479620 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/20
Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA - Mwanaume mmoja wa eneo la New Jersey Marekani amekiri kutenda uhalifu wa chuki kwa kuharibu kituo cha wanafunzi wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Rutgers mapema mwaka huu, maafisa walitangaza Alhamisi.
Habari ID: 3479575 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/11
Ubaguzi Marekani
IQNA - Kundi la kutetea haki za Waislamu Marekani limewasilisha malalamiko katika Idara ya Elimu ya Marekani, likitaka uchunguzi ufanyike iwapo Chuo Kikuu cha Michigan kimeshindwa kuwalinda wanafunzi wa Palestina, Waarabu, Waislamu na Waasia Kusini kutokana na kubaguliwa.
Habari ID: 3479574 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/10/11
Dhulma
IQNA - Mahakama ya Kuu ya Marekani, mfumo wa mahakama ya Missouri na Gavana wa jimbo hilo Michael Lynn Parson wamelaaniwa kwa kushindwa kuzuia kunyongwa kwa mfungwa Mwislamu aliyehukumiwa kifo kimakosa.
Habari ID: 3479493 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/09/26
Arbaeen
IQNA - Mwakilishi wa Jimbo la Utah nchini Marekani Trevor Lee amehimizwa kukutana na Waislamu wa jimbo hilo baada ya video aliyochapisha kusababisha wimbi la chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3479351 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/30
Waislamu Marekani
IQNA - Polisi wa Marekani mjini New York (NYPD) walirarua hijabu za wanawake wengi wa Kiislamu waliokuwa wakiandamana nje ya mkutano wa kukusanya fedha wa Kamati ya Kitaifa ya chama cha Democrat wiki iliyopita.
Habari ID: 3479317 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/23
Watetezi wa Palestina
IQNA - Kundi la kutetea haki za Waislamu Marekani limetangaza kesi dhidi ya serikali ya shirikisho kwa kuwaweka Wapalestina-Wamarekani wawili kwenye orodha ya siri ya kufuatiliwa kutokana na msimamo wao wa kuwaunga mkono Wapalestina wanaoteswa na Israel huko Gaza.
Habari ID: 3479272 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/08/13
Waislamu Marekani
IQNA – Ofisi ya Maadili ya Chuo Kikuu cha Duke nchini Marekani imeanzisha uchunguzi kuhusu uchafuzi wa mabango kuhusu mwezi wa Ramadhani, jambo ambalo limeibua wasiwasi wa chuki dhidi ya Uislamu ndani ya a chuo hicho.
Habari ID: 3478750 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/30