IQNA

Warsha ya Arubaini yafanyika Bauchi, Nigeria

13:24 - November 19, 2015
Habari ID: 3454535
Warsha ya kuhusu kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein AS imefanyika Bauchi nchini Nigeria.

Warsha hiyo iliyofanyika Jumapili iliyopita imefanyika kwa lengo la kuimarisha hatua za usalama na nidhamu wakati wa maadhimisho ya Arubaini.

Kati ya viongozi waandamizi walioutubu katika kikao hicho ni Amir wa Bauchi, Sheikh Ahmad Yusuf Yashi.


Wahadhiri kutoka maeneo mbali mbali walihutubu katika warsha hiyo ambapo walihutubu kuhusu maadili meme, udugu, kuzingatia nidhamu wakati wa ibada na pia kulionyeshwa mkanda wa video wa hotuba ya kiongozi wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia nchini Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaki katika maadhimisho ya Arubaini mwaka uliopita.
Ikumbukwe kuwa takribani miaka 1376 iliyopita, ilifanyika majlisi ya kwanza ya siku ya Arubaini tangu kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) Imam Hussein bin Ali (AS) akiwa na watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume ambao waliuawa shahidi tarehe 10 Muharram mwaka 61 Hijria. Majlisi za siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala.../

3454149

captcha