IQNA

Ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu Ufaransa

6:38 - November 22, 2015
Habari ID: 3455375
Vitendo vya chuki na utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa vinaripotiwa kuongezeka siku baada ya siku hasa baada ya mashambulio ya kigaidi ya hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo Paris.

Makundi mawili ya kutetea haki za binadamu nchini Ufaransa yametangaza kuwa, vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu nchini humo vimeshadidi baada ya mashambulio ya kigaidi mjini Paris. Abdallah Zekri Mkuu wa Kituo cha Kupambana na Vitendo vya Kuuonesha Uislamu kuwa ni tishio amesema kuwa, vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu nchini humo vimeongezeka na kwamba, kwa wiki kumekuwa kukiripotiwa kesi nne hadi tano za vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu katika nchi hiyo ya Ulaya. Yasser Louati msemaji wa kituo kingine cha kutetea haki za Waislamu nchini Ufaransa na kupambana na vitendo vya kuufanya Uislamu uogopwe amesema kuwa, baada ya mashambulio ya kigaidi ya Paris kumeripotiwa makumi ya kesi za utumiaji mabavu dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu nchini humo. Ufaransa ina Waislamu milioni tano ambao wanaunda asilimia nane ya wakazi wa nchi hiyo.

3454905

captcha