IQNA – Utafiti mpya wa kitaifa umebaini kuwa Waislamu nchini Ufaransa wanaripoti viwango vya juu zaidi vya ubaguzi wa kidini kuliko makundi mengine yote.
Habari ID: 3481619 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/06
IQNA – Baraza Kuu la Waislamu Ufaransa (CFCM) limesema waumini wameshtushwa na kuumizwa sana baada ya mtu kuvamia msikiti ulioko kusini-kati mwa Ufaransa na kurarua nakala za Qur’ani Tukufu kisha kuzitupa chini.
Habari ID: 3481605 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/02
IQNA – Waziri wa Ndani wa Ufaransa amepinga jaribio jipya la kupiga marufuku Hijabu kwa wasichana wadogo katika maeneo ya umma, akionya kuwa mpango huo unaweza kuwalenga kwa dhulma vijana Waislamu.
Habari ID: 3481598 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/01
IQNA – Mohamed Ameur Ghedira alikuwa profesa mashuhuri katika Chuo Kikuu cha Lyon aliyetarjumu Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa.
Habari ID: 3481591 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/30
IQNA – Mashirika kadhaa ya Kiislamu nchini Ufaransa yamekosoa taasisi ya utafiti wa maoni ya wananchi, IFOP, kwa kile walichokiita upendeleo wa wazi na kuvunja viwango vya maadili ya kitaaluma.
Habari ID: 3481564 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/25
IQNA – Baraza la Imani ya Kiislamu Ufaransa (CFCM) limepinga vikali utafiti mpya wa taasisi ya Ifop, likisema utafiti huo unachochea unyanyapaa na kuendeleza chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu (Islamophobia)
Habari ID: 3481548 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/21
IQNA – "Misikiti katika Uislamu" ni jina la maonyesho ya sanaa yaliyozinduliwa katika Msikiti Mkuu wa Paris, mji mkuu wa Ufaransa.
Habari ID: 3481379 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/18
IQNA – Waislamu wawili kati ya watatu nchini Ufaransa wanasema wamekumbwa na tabia za kibaguzi, kwa mujibu wa utafiti mpya unaoangazia ubaguzi mpana katika ajira, makazi, na huduma za umma.
Habari ID: 3481246 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/17
IQNA – Mamlaka za Ufaransa zimeanzisha uchunguzi kufuatia jaribio la kuchoma moto chumba cha kusalia cha Waislamu mjini Châtillon-sur-Seine, tukio ambalo maafisa wamelilaani kuwa ni kitendo cha kigaidi cha uoga na chenye chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3481095 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/16
IQNA – Mwanaume mwenye umri wa miaka 27 nchini Ufaransa amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa kitendo cha kuvunjia heshima Qur'ani, Kitabu Kitakatifu cha Uislamu.
Habari ID: 3481024 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/01
IQNA – Mamlaka za Ufaransa zimeripoti ongezeko la asilimia 75 la matukio ya chuki dhidi ya Waislamu katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2025, huku mashambulizi dhidi ya watu binafsi yakiongezeka mara tatu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Habari ID: 3480892 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/04
IQNA – Serikali ya Ufaransa imeshutumiwa kwa kulenga shirika la Ulaya linalojitolea kupambana na chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3480767 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/31
IQNA – Baraza la Kiislamu la Ufaransa (CFCM) limeitaka Ufaransa na Umoja wa Ulaya kuitambua rasmi Palestina kama nchi huru na kusitisha makubaliano yao ya kisiasa na kiuchumi na utawala wa Israel kutokana na jinai za utawala huo huko Gaza.
Habari ID: 3480716 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/21
IQNA – Maelfu ya watu wameandamana katika mitaa ya Paris na miji mingine ya Ufaransa siku ya Jumapili kulaani ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu na kumuenzi Aboubakar Cissé, kijana kutoka Mali aliyeuawa akiswali ndani ya msikiti.
Habari ID: 3480675 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/12
IQNA-Mwanaume mmoja wa Kifaransa aliyemdunga kisu na kumuua Mwislamu aliyekuwa akisali katika msikiti ulioko kusini mwa Ufaransa, ameshtakiwa rasmi kwa mauaji ya kukusudia yanayochochewa na chuki ya kidini au kikabila, ofisi ya mwendesha mashtaka wa Nîmes ilitangaza Ijumaa.
Habari ID: 3480667 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/11
IQNA – Italia imemrudisha Ufaransa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji ya kijana Mwislamu katika msikiti wa Ufaransa.
Habari ID: 3480664 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/10
IQNA – Muungano mpana wa makundi ya kisiasa, mashirika ya kiraia, wasomi, watafiti, waandishi na watu mashuhuri umetangaza maandamano ya kimya yatakayofanyika kote Ufaransa Jumapili, Mei 11, kulaani kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia).
Habari ID: 3480659 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/09
IQNA – Wabunge wa Ufaransa siku ya Jumanne walikusanyika kwa heshima kuu kumkumbuka Muislamu aliyepoteza maisha katika shambulio la kusikitisha ndani ya msikiti uliopo kusini mwa nchi hiyo.
Habari ID: 3480619 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/30
IQNA – Wanamichezo wanawake wa Kiislamu nchini Ufaransa wamejitokeza kupinga muswada mpya wa sheria unaolenga kupiga marufuku uvaaji wa Hijabu katika mashindano ya michezo ya kitaifa, wakisema hatua hiyo inakiuka uhuru wa dini na kujieleza.
Habari ID: 3480491 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/04
IQNA-Baraza la Kiislamu la Ufaransa (CFCM) limelaani kampeni inayoenea inayolenga wanawake wa Kiislamu wanaovaa hijabu, likiitaja kama yenye madhara na inayodhoofisha mshikamano wa kitaifa.
Habari ID: 3480455 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/28