IQNA

Watu 13 wauawa katikamlipuko ndani ya Msikiti nchini Cameroon

19:33 - January 13, 2016
Habari ID: 3470039
Watu wasiopungua 13 wameuawa baada ya kutokea hujuma ya bomu ndani ya msikiti mmoja, kaskazini mwa Cameroon.

Maafisa wa masuala ya usalama nchini Cameroon wamesema shambulio hilo limetokea katika eneo la Kolofata karibu na mpaka wa nchi hiyo na Nigeria. Imearifiwa kuwa watu 13 wameuawa na mwengine mmoja kujeruhiwa kwenye shambulio hilo la kigaidi.

Ingawa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na shambulio hilo, lakini kidole cha lawama kinaelekezwa kwa magaidi wakufurishaji wa Boko Haram ambao ndio wanaohusika na mashambulizi yanayoshabihiana na hayo katika nchi za Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.

Kwa muda wa miaka sita sasa kundi la kigaidi Boko Haram linafanya mashambulizi dhidi ya Waislamu na Wakristo na taasisi za serikali nchini Nigeria na sasa kundi hilo la wakufurishaji limepanua hujuma zake hadi katika nchi jirani,

Hadi hivi sasa zaidi ya watu 20 elfu wameshauwa, mamia ya maelfu ya wengine kujeruhiwa na wengine wengi kuwa wakimbizi ndani na nje ya eneo hilo la magharibu mwa Afrika kutokana na mashambulizi ya magaidi wa Boko Haram.

3467235

captcha