IQNA

Qarii mashuhuri wa Misri, Sheikh Mustafa Ghalwash aaga dunia

16:13 - February 04, 2016
2
Habari ID: 3470115
Qarii wa kimataifa wa Misri, Sheikh Ragheb Mustafa Ghalwash ameaga dunia Alhamisi hii akipata matibabu hospitalini nchini Misri.
Qarii mashuhuri wa Misri, Sheikh Mustafa Ghalwash aaga dunia
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tovuti ya elwehda.com, Sheikh Mustafa Ghalwash aliyekuwa qarii katika Radio ya Qur'ani ya Misri na mwanachama wa Jumuiya ya Wasomaji (quraa) na Waliohifadhi (huffadh) Qur'ani Misri ameaga dunia na kurejea kwa Mola wake mapema leo alfajiri akiwa na umri wa miaka 77 katika moja ya hospitali za Misri.

Sheikh Taha Noomani, mwanachama wa Jumuiya ya Wasomaji na Waliohifadhi Qur'ani Misri amesema Sheikh Mustafa Ghalwash atazikwa leo baada ya sala ya Alasiri katika kijiji alikozaliwa cha Borma katika mkoa wa Gharbiya nchini Misri. Ameongeza kuwa Ijumaa kutafanyika khitam ya marhuma Sheikh Mustafa Ghalwash katika kijiji hicho.

Ghalwash aliwahi kualikwa kusoma Qur'ani katika nchi mbali mbali kama vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Uingereza, Ufaransa na Marekani.

Kuhusu kumbukumbu yake ya safari nchini Iran Ghalwash alisema: "Sijawahi kuona watu wenye kusikilizaj qiraa ya Qur'ani kwa hisia ya dhati ya moyo kama nilivyoona Iran. Naona mustakabali mzuri kwa maquraa nchini Iran kwani wana lahni na tajwidi nzuri sana."

Qarii mashuhuri wa Misri, Sheikh Mustafa Ghalwash aaga dunia
Sheikh Ghalwash akimpa mkono Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
katika moja ya safari zake Iran.



3472883

Imechapishwa: 2
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Bila jina
0
0
Allahummaghfirlah
hassan ibrahim.
0
0
la haula wala kuwata illa billah!!!!!!.
captcha