IQNA

Kiongozi Muadhamu atoa wito kwa Wairani kushiriki kwa wingi katika upigaji kura

16:04 - February 26, 2016
Habari ID: 3470163
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa wito kwa Wairani kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa leo wa Bunge na Baraza la Wanazuoni Wataalamu lilalomchagua Kiongozi Muadhamu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa wito huo leo muda mfupi baada ya kupiga kura yake na kubainisha kwamba, kushiriki katika uchaguzi ni haki na jukumu la kila Muirani. Amesisitiza kwamba, uchaguzi unapaswa kufanyika kwa namna ambayo itamkatisha tamaa na kumvunja moyo adui. Ayatullah Khamenei sambamba na kuashiria kwamba, chaguzi za leo hapa Iran za Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchangua Kiongozi Muadhamu na kusimamia kazi zake zina umuhimu mkubwa amesema kuwa, kila mtu anayependa izza ya Kiislamu na adhama ya kitaifa anapaswa kushiriki katika uchaguzi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, katika Uislamu na maarisho yake kufanya haraka katika jambo la kheri ni suala ambalo limeusiwa na kwa msingi huo wananchi wanapaswa kuharakisha kuelekea katika masanduku ya kupigia kura; hata hivyo hii haina maana ya kufanya mambo kwa kukurupuka.

Amesema, kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita, wananchi wa Iran leo pia wanapaswa kujitokeza kwa wingi na kuwachagua wawakilishi wao wa Bunge na Baraza la Wanazuoni wanaomchagua Kiongozi Muadhamu.

3478308

captcha