Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tovuti ya ‘Nujumu Misriya’ imeandika kuwa: "Kuna magonjwa mengi sugu ambayo tiba yake iko mbele ya macho ya mwanadamu lakini kutokana na kughafilika husumbuka akitafuta tiba kwa magonjwa hayo.”
Tovuti hiyo imeendelea kuandika kuwa, "Mwenyezi Mungu SWT ameitaja Qur’ani kitabu kilichoteremshwa kwa ajili ya tiba au shifaa kwa watu na rehema kwa walimwengu wote. Kwa kusoma kwa makini Kitabu hiki kitukufu na kusoma hadithi za Mtume SAW na aliyoamiliana na Masahaba zake basi tutaweza kufahamu zaidi Wahyi.”
Ugonjwa kupoteza fahamu au Alzheimer huwaathiri watu wengi hasa wazee katika maeneo mbali mbali duniani.
Ugonjwa wa Alzheimer na magonjwa mengine ya kiakili yanaweza kutibiwa kwa kusoma Sura Yassin katika Qurani tukufu.
Tovuti ya ‘Nujumu Misriya’ inafafanua zaidi kwa kuandika: "Baada ya kuaga dunia Mtume wa Uislamu SAW, Ibn Abbas (sahaba na mtoto wa ami yake Mtume SAW) alikuwa ameketi ndani ya Msikiti kasha mtu akaingia akipiga kilele huku akitamka maneno yasiyoeleweka. Waliokuwa ndani ya msikiti wakainuka ili kumfukuza mtu huyo; hapo Ibn Abbas akawauliza hadhirina kwa nini walichukua hatua hiyo nao wakajibu kwa kusema amepoteza akili na hajui asemacho. Ibn Abbas akainuka na kuweka mikoni yake miwili juu ya kichwa cha mgonjwa huyo na kisha akasoma Sura Yassin. Baada ya kusomewa Sura Yassin mgonjwa akainuka na afya yake ikarejea kama kawaia na akawa haugui chochote. Ibn Abbas aliulizwa ni kipi alichokifanya hadi mtu huyo akapona. Alijibu kwa kusema: ‘Mtume SAW aliitaja Sura Yasin kuwa ‘Moyo wa Qur’ani’ na ndio niliyomsomea.”
Abdullah ibn Abbas bin Abdul Muttalib bin Hashim bin Abdul Manaf maarufu kama Ibn Abbas ni mtoto wa Abbas bin Abdul Mutalib ami yake Mtume (SAW) na alikuwa pia sahaba na msaidizi wa Imam Ali AS.
Ibn Abbas anatambuliwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni kama aliyekuwa mcha Mungu, mwenye ulimu, ujuzi na heikima. Katika zama za ujana wake alimhudumia Mtume SAW na vitabu vingi vyenye itibari vya hadithi vimenukulu hadhiti kutoka kwake.
Ibn Abbas alikuwa mataalamu katika kufasiri Qur’ani.