IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran kuanza Mosi Ramadhani

12:56 - May 31, 2016
Habari ID: 3470349
Maonyesho ya 24 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanatazamiwa kuanza mjini Tehran katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam Mohammad Heshmati, Mkuu wa Kitengo cha Qur'ani Katika Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu alipozungumza na waandishi habari mjini Tehran Jumatatu hii.

Sheikh Heshmati amesema maonyesho ya Qur'ani ni fursa ya wanaharakati wa Qur'ani kukutana na kutumia uwezo wao ili watu waweze kuifahamu Qur'ani zaidi.

Amesema kaulimbiu ya maonyesho ya mwaka huu ni "Kuelekea Katika Ufahamu wa Qur'ani."

Aidha amesema kufahamu Qur'ani hupelekea kutekelezwa mafundisho yake na kwa hivyo lengo kuu la maonyesho ni kuwahimiza watu kusaidiana katika kufahamu vyema zaidi mafundisho ya Qur'ani.

Amesema maonyesho ya mwaka huu yatakuwa na vibana 300 huku kitengo cha vitabu kikiwa kikubwa zaidi.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran ni makubwa zaidi ya aina yake duniani.

Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran ambapo huwa na vitengo kadhaa vya maudhui mbali mbali za Qur'ani.

3459962

captcha