IQNA

Iran yaalika nchi 70 katika mashindano ya Qur'ani ya wanafunzi wa shule

15:30 - February 12, 2017
Habari ID: 3470846
IQNA: Iran imealika nchi 70 kushiriki katika Mashindano ya Tano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya wanafunzi wa shule.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Wizara ya Elimu ya Iran imesema nchi 20 hadi sasa zimetangaza kuwa tayari kutuma washiriki katika mashindano hayo ya Qur'ani.

Kwa mujibu wa ratiba iliyopo, mashindano hayo yatafanyika kwa munasaba wa Mabaath ya Mtume SAW tarehe 27 Rajab.

Wizara ya Elimu ya Iran imesema mashindano hayo yatakuwa na kategoria mbili za qiraa au kusoma na kuhifadhi Qur'ani kikamilifu.

Wawakilishi wa Iran katika mashindano hayo wamechaguliwa baad aya duru kadhaa za mashindano ya shule za msingi na upili katika miji, mikoa na hatimaye ngazi ya kitaifa.

Mashindano hayo ambayo lengo lake ni kuimarisha utamaduni wa Qur'ani miongoni mwa wanafunzi yanaandaliwa na Shirika la Awqaf la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

3573376


captcha