Jaji James Wakiaga ametoa hukumu na kusema kuwa sera iliyoanzishwa na shule hiyo mnamo Januari 2019 ya kuwanyima wanafunzi Waislamu haki ya kidini ya kuswali Adhuhuri kwa madai ya kuwepo wasiwasi wa usalama ilikiuka haki ya kidini wanafunzi Waislamu mbali na kuwanyima haki ya elimu na haki ya kutobaguliwa, na kuwaweka katika hali mbaya miongoni mwa wanafunzi wengine.
Menejimenti ya shule ilitetea sheria hizo, ikidai kuwa ililenga kuhimiza utangamano na mshikamano miongoni mwa wanafunzi ili kukuza ubora.
Oshwal Academy iliongeza kuwa lengo la miongozo hiyo ni kutoruhusu udhihirisho wowote wa dini yoyote na kwamba sera hili ilikubalika kwa wengi wa wazazi na kupingwa na wachache.
Lakini jaji huyo alisema ingawa haki ya dini chini ya Kifungu cha 32 cha Katiba ya Kenya si kamilifu, kizuizi chochote lazima kiwe kwa mujibu wa sheria kuu.
Kesi hiyo iliwasilishwa na mzazi wa zamani wa shule hiyo ambaye alitaka kulinda haki ya msingi ya elimu na uhuru ya dini kwa wanafunzi wa Kiislamu ambao walitaka kutekekeleza faradhi ya Swala kama inavyotakiwa katika imani ya Kiislamu.
Mohamed Khan alisema aliwasilisha ombi hilo kwa niaba ya wanafunzi wa Kiislamu, akipinga uamuzi wa shule kuwapiga marufuku kuswali ndani ya eneo la shule.
3490989