IQNA

Waislamu

Mbunge wa Ufaransa ashtakiwa na shule ya Waislamu kwa uzushi

20:48 - December 18, 2024
Habari ID: 3479915
IQNA - Shule ya Kiislamu kusini-mashariki mwa Ufaransa imewasilisha kesi mahakamani dhidi ya mbunge kwa kuibua uzushi dhidi ya shule hiyo

Shule ya kibinafsi ya Al-Kindi, ambayo ni ya Waislamu huko Décines-Charpieu, wilaya katika mkoa wa Lyon kusini-mashariki mwa Ufaransa, inamshtaki mbunge huyo baada ya mwanasiasa huyo kuishutumu shule hiyo kwa "kukanusha historia" na kutowafundisha wanafunzi kuhusu kile kinachotajwa kuwa ni Holocaust (mauaji ya Wayahudi katika vita vya pili vya dunia nchini Ujerumani)

Shule imekanusha vikali shutuma hizi na kusema madai ya mwanasiasa huyo ni ya uwongo na yana madhara, na kuyataja kuwa "jaribio la kuharibu sifa yake." Shule hiyo ilionya zaidi kwamba haitaacha "uongo huu kwenda bila kuadhibiwa" na hivyo imechukua hatua ya kisheria.

Al-Kindi imetetea rekodi yake katika kukuza ufahamu wa kihistoria.

Laurent Wauquiez, kutoka chama cha Les Républicains, anakabiliwa na mashtaka ya kulenga kuzua utata na kushawishi ukaguzi unaoendelea wa kuwezesha shule hiyo kupata ufadhili wa serikali.

Al-Kindi ni shule ya mwisho ya Waislamu ya kibinafsi nchini Ufaransa inayofanya kazi chini ya kandarasi ya serikali. Imekuwa chini ya uchunguzi mkali kutoka kwa mamlaka za mitaa mwaka huu, na imefanyiwa  ukaguzi wa kushtukiza.

Viongozi wanashutumu shule hiyo kwa makosa ya kifedha na ufundishaji, ikiwa ni pamoja na madai kwamba fedha zilizokusudiwa kwa madarasa yaliyoidhinishwa na serikali zilitumika kwa shughuli ambazo hazijaidhinishwa. Pia wanasema baadhi ya vitabu vya shule hiyo vinataja "jihad" kwa njia inayodaiwa kuwa inatia wasiwasi na wanasema kuwa baadhi ya vitabu vinachochea mapambano dhidi ya ushoga.

Shule hiyo imetaja shutuma hizo kuwa hazina msingi, hasa ikipinga madai kwamba baadhi ya vitaby vya kufundishia vinachochea itikadi kali. Inaeleza kwamba neno “jihad” limewasilishwa katika baadhi ya vitaby kama mapambano ya kibinafsi au ya kiroho, si kama mwito wa vita vya silaha.

Wakaguzi hapo awali waliikosoa shule hiyo kwa kanuni zake za mavazi, zinazopiga marufuku vipodozi na mavazi yasiyofaa kwa wasichana.

Shirikisho la Kitaifa la Shule za Kibinafsi za Kiislamu (FNEM) limejitokeza kuunga mkono Al-Kindi, likishutumu serikali kwa kulenga shule za Kiislamu isivyo haki. FNEM imesema shule za Kikatoliki chini ya kandarasi sawa hazikabiliwi na kiwango sawa cha mashinikizo na ukaguzi.

Katika taarifa, Rais wa FNEM Makhlouf Mameche alionya kwamba kuondoa kandarasi ya shule hiyo kunaweza kuharibu miaka ya kazi ngumu.

Kikao cha Desemba 12 kiliruhusu pande zote mbili kuwasilisha hoja, huku shule hiyo ikidumisha dhamira yake ya kutetea sifa yake nzuri na kupigania kuweka ufadhili wake wa serikali kuendelea kuwahudumia wanafunzi.

3491093

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hijab ufaransa shule
captcha