IQNA

Roboti ya kusafisha Msikiti yaundwa Uturuki

16:03 - May 30, 2018
Habari ID: 3471537
TEHRAN (IQNA) – Kutokana na Waislamu kuswali mara tano kwa siku katika sala za jamaa misikitini, suala la usafi na unadhifu ni muhimu sana na limetiliwa mkazo katika mfundisho ya Kiislamu.

Kwa msingi huo shirika moja la Uturuki linalojulikana kama Turnaco Robotik limetumia teknolojia kwa lengo la kuboresha unadhifu na usafi katika misikiti. Shirika hilo limeunda roboti ya kipekee duniani ya aina yake yenye uwezo wa kusafisha mikeka misikitini. Mkurugenzi wa Turnaco Robotik Kerem Sencan anazungumza kuhusu roboti hiyo iliyopewa jina la "Mouro" kwa kusema: "Mfumo wa usafishaji wa roboti hii husafisha zulia na kuondoa vijidudu kwa kutumia miale ya UVC na gesi ya ozone. Huondoa harufu mbaya na unaweza kuisimamia roboti hiyo kwa aplikesheni ya simu za mkononi."

Anasema fikra ya kuunda roboti hiyo ilimjia wakati alipomsikia mzee aliyekuwa na matatizo ya kupumua akilalamika kuwa alikuwa wakikumbwa na matatizo kila alipoenda katika misikitini.

Anasema madaktari walimfahamisha kuwa kuenda msikiti huathiri afya yake vibaya kutokana na kuwa mazulia yalikuwa yakitumiwa na watu wengi na kusalia muda mrefu bila kusafishwa. "Aidha katika misikiti ambayo mimi husali katika eneo la  Kadıköy huwa na harufu isiyo nzuri." Nilizungumza na Imamu na akanifahamisha kuwa kuna tatizo katika  kusafisha mazulia ya msikiti na hivyo husafishwa mara moja kwa mwezi. Anasema kwa msingi huo aliamua kuunda roboti ambayo inaweza kusafisha mazulia ya msikiti kila siku sambamba kuhakikisha kuwa daima yanakuwa masafi na yenye harufu nzuri.

3465983

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha