IQNA

Kitabu cha 'Muziki katika Uislamu' chachapishwa Misri

20:06 - August 24, 2018
Habari ID: 3471644
TEHRAN (IQNA)- Kitabu chenye anuani ya "Muziki katika Uislamu" kilichoandikwa na Dkt. Suhair Abdel-Azim kimechapishwa nchini Misri.

Kitabu hicho ambacho kimechapishwa na Idara ya Vituo vya Utamaduni Misri kinachunguza masula ya muziki katika dini tukufu ya Kiislamu tokea kudhihiri dini hii hadi karne ya 20.

Mwandishi wa kitabu hiki anasema kuna uhusiano wa karibu baina ya sanaa na dini ya Kiislamu. Anaongeza kuwa Sanaa inainua hisia na irada na dini nayo ambayo ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu imekuja ili imfikishwe mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu. Aidha anaashiria ukuruba uliopo baina ya muziki na tartili pamoja na tajwidi ya Qurani Tukufu. Halikadhalika kitabu hicho kimeangazia pia historia ya muziki,  na pia masuala ya kususiwa na kutosusiwa muziki katika Uislamu.

Kumekuwepo na mjadala wa kifiqhi kwa muda mrefu baina ya wanazuoni wa Kiislamu kuhusu uhalali au uharamu wa muziki. Baadhi ya wanazuoni wanasema muziki bila ala za muziki ni halali huku baadhi wakisisitiza kuwa ala za muziki zinaruhusiwa maadamu aina ya muziki na utumiaji wa ala ni kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

3740856

captcha