
Kwa mujibu wa tovuti ya Cairo24, wawakilishi kutoka nchi 30 wanashiriki katika toleo hili la mashindano. Jumla ya washiriki 42 wakiwemo maqari, wahifadhi wa Qur'ani Tukufu na waimbaji wa Ibtihal wanashindana katika mashindano hayo.
Mashindano haya yamepewa jina la marehemu msomaji mashuhuri wa Misri, Sheikh Mahmoud Ali Al-Banna, kwa heshima ya mchango wake mkubwa na wa kudumu katika kuhudumia Qurani Tukufu.
Siku ya kwanza ya mashindano ilijumuisha Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Salam mjini Port Said, pamoja na tilawa mbalimbali za Qurani, dua, na nyimbo za kidini zilizofanyika katika viwanja na mitaa kadhaa ya mji huo.
Hafla rasmi ya ufunguzi ilifanyika saa 12:00 jioni kwa saa za huko, ikihudhuriwa na Waziri wa Awqaf wa Misri, Gavana wa Port Said, maafisa wa Al-Azhar, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa serikali.
Habari inayohusiana:
Tukio hili limeandaliwa kwa msaada wa Waziri Mkuu wa Misri, Mustafa Madbouly.
Mashindano ya Qurani ya Port Said yataendelea hadi tarehe 2 Februari 2026, ambapo washiriki watashindana katika nyanja za kuhifadhi Qur'ani, usomaji (tilawa), na Ibtihal.
4331302