IQNA

Inna Lillah wa Inna Ilayi Rajioun
22:45 - September 19, 2019
News ID: 3472139
TEHRAN (IQNA) - Watoto wasiopungua 27 wamepoteza maisha nchini Liberia baada ya madrassah ya yao ya bweni kuteketea moto nje ya mji mkuu Monrovia.

Kwa mujibu wa taarifa, watoto walikuwa wamelala wakati shule yao ilipoanza kuteketea Jumanne usiku. Madrassah ambayo imekumbwa na mkasa huo wa moto ilikuwa maalumu ya kufunza Qur'ani Tukufu. Msemaji wa Polisi ya Liberia Moses Carter amesema bado hawajaweza kubaini chanzo cha moto huo uliojiri katika mji wa Pyanesville. Taarifa zinasema waalimu wawili pia wamepoteza maisha katika tukio hilo la kusikitisha.
Rais George Weah wa Liberia ametuma salamu zake za rambi rambi kufuatia msiba huo na kusema huu ni wakati mgumu kwa taifa la Liberia na familia za waathirika. Aidha Rais Weah ametembelea eneo la maafa na kujiunga na waathirika katika maombolezo.
Serikali ya Liberia imetangaza maombolezo ya kitaifa kufuatia maafa hayo huku uchunguzi ukiwa umeanza kubaini sababu zilizopelekea watoto hao pamoja na walimu wao kuaga dunia.
Wote walioaga dunia katika tukio hilo walizikwa Jumatano mchana.

3469441

Name:
Email:
* Comment: