IQNA

Waislamu 40 wauawa katika mapigano Jamhuri ya Afrika ya Kati

11:20 - December 30, 2019
Habari ID: 3472315
TEHRAN (IQNA) – Waislamu wasiopungua 40wameuawa katika mapigano yaliyojiri hivi karibuni huko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Taarifa zinasema mapigano yalianza Jumanne 24 Disemba katika mtaa wa PK5 baada ya wanamgambo kuhujumu biashara za Waislamu.

Sheikh Awad al Karim, Imamu wa Msikiti wa Ali Babolo katika mtaa huo, ambao aghalabu yake ni Waislamu, amesema waliipokea miili ya Waislam waliouawa na kuandaa mazishi kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Inakadiriwa kuwa baina ya maduka 40 hadi 50 ziliteketezwa moto katika hujuma hiyo ambayo imeulengaa mtaa wa PK5 ambao uligeuka kuwa makao ya Waislamu wakati walipokuwa wakishambuliwa na genge la Kikristo la Anti-Balaka miaka michache iliyopita.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) yaliibuka mwaka 2013, baada ya waasi wa Seleka kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo,François Bozizé. Baada ya rais Mwislamu, Michel Djotodia kuchukua mamlaka, waasi na magaidi wa Kikristo wenye kufurutu ada wa Anti-Balaka walianzisha mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Waislamu, ambapo maelfu waliuawa na wengine wengi kuwa wakimbizi.

Djotidia alilazimishwa na nchi za kieneo kujiuzulu Januari mwaka 2014 na hapo mauaji ya Waislamu yakashika kasi zaidi. Kabla ya kuanza mgogoro, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, ulikuwa na wakaazi 130,000 Waislamu lakini sasa taarifa zinasema idadi hiyo ni chini ya 1,000.

Aidha watu zaidi ya 400,000, wengi wakiwa ni Waislamu wamelazimika kukimbia makazi yao huku misikitr 436 kati ya misikiti yote 417 ya nchi hiyo ikiharibiwa au kubomolewa katika vita hivyo.

20191226

captcha