IQNA

16:29 - January 20, 2020
News ID: 3472389
TEHRAN (IQNA) – Mohammad Moussaoui amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Baraza la Waislamu Ufaransa (CFCM).

Katika mkutano uliofanyika Jumpili katika Msikiti wa Jamia wa Paris, wanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa CFCM waliwachagua viongozi wa baraza hilo ambapo nafasi zilizojazwa ni za mwenyekiti, makamu wenyekiti, katibu mkuu na mweka hazina.

Nafasi ya mwenyekiti imechukuliwa na mgombea pekee ambaye alikuwa ni Mohammad Moussaoui, raia wa Ufaransa mwenye asili ya Moroco. Alipata ushindi baada ya mshindani wake mwingine, Chems Eddine Hafiz, ambaye ni Mfaransa mwenye asili ya Algeria kutangaza kujitoa katika uchaguzi ili aweze kutekeleza jukumu lake kama Imamu wa Msikiti wa Jamia wa Paris.

Moussaoui pia ni rais wa Jumuiya ya Misikiti ya Ufaransa. Baraza la Waislamu Ufaransa (CFCM) lilibuniwa na serikali ya Ufaransa mwaka 2003 kwa lengo la kutoa ushauri na muongoni kwa serikali na taasisi zote za umma kuhusu masuala ya Uislamu na Waislamu. CFCM huleta pamoja jumuiya mbali mbali za Waislamu. Kuna takribani Waislamu milioni 6 nchini Ufaransa.

3470404

 

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: