IQNA

Maandamano ya Siku ya Kupambana na Ubeberu yafanyika kote Iran

20:08 - November 04, 2025
Habari ID: 3481465
IQNA-Maandamano ya Siku ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu yaani Aban 13 ambayo ni Siku ya Taifa ya Iran ya Kupambana na ubeberu na uistikbari yamefanyika hapa mjini Tehran na katika zaidi ya miji 900 kote humu nchini.

Aban 13  ambayo ni kumbukumbu ya harakati ya wanafunzi wa Iran ya kuuteka ubalozi wa Marekani uliokuwepo Tehran  kutokana na ubalozi huo kufanya ujasusi mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 nchini Iran, yalianza saa tatu asubuhi kwa saa za hapa Tehran katika miji zaidi ya 900 kote nchini Iran. Kwa hapa Tehran, kituo cha kuanzisha maandamano hayo kimekuwa ni  Uwanja wa Palestina kuelekea Mtaa wa Taleghani kwenye pango la kijasusi yaani sehemu ulipokuwepo ubalozi wa Marekani hapa Tehran.

Kaulimbiu kuu ya maandamano hayo ni kupinga ubeberu na uistikbari hasa wa Marekani. Skuli 120,000 za Iran zimepiga kengele za kuadhimisha siku hii huku walimu wakuu na wakuu wa skuli zote wakishiriki kikamilifu katika maandamano ya leo ya wanafunzi kote nchini Iran. Tarehe 13 Aban (4 Novemba) inafahamika katika kalenda ya Iran kama "Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari Duniani".

Siku hii inasadifiana na kumbukumbu ya kutekwa "Pango la Ujasusi" la uliokuwa ubalozi wa Marekani hapa mjini Tehran mnamo mwaka 1979. Tukio hili halikuwa ni jibu tu kwa Marekani kuendelea kuingilia masuala ya ndani ya Iran, bali pia ilikuwa ni hatua ya mabadiliko katika mwamko wa kisiasa wa taifa la Iran na nembo ya mshikamano wa kitaifa dhidi ya siasa za kupenda kujitanua za nchi za Magharibi. 

Ubalozi wa Marekani mjini Tehran, ambao ulikuwa "Pango la Ujasusi" ulijulikana kama kituo cha kubuni na kutekeleza mipango ya kijasusi, kisiasa na kiusalama dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Nyaraka zilizopatikana ndani ya ubalozi huo zilifichua uingiliaji mkubwa wa Marekani katika masuala ya ndani ya Iran kuanzia zama za Pahlavi hadi baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Miongoni mwa mambo muhimu zaidi ya uingiliaji kati huu ilikuwa nafasi ya moja kwa moja ya Marekani katika mapinduzi ya Agosti 19, 1953, na uungaji mkono wake usio na masharti kwa utawala dhalimu. Kufichuliwa kwa nyaraka hizi kulidhihirisha sura halisi ya sera za Marekani kwa watu wa Iran na walimwengu, na kulionyesha kwamba balozi zinaweza kuwa msingi wa ujasusi na njama dhidi ya mataifa.

Kutekwa ubalozi wa Marekani lilikuwa ni vuguvugu la hiari lililoibuka kutoka kwa jamii ya wanamapinduzi ya Iran. Kwa hatua hiyo, wanafunzi wanaofuata fikra za Imam Khomeini (RA) hawakuonyesha tu upinzani wao dhidi ya siasa za uingiliaji kati za Marekani, bali pia walifungua njia ya kuanzishwa kwa msamiati wa "chuki dhidi ya ubeberu" katika fasihii ya kisiasa ya mapinduzi. Kwa hakika tarehe 13 Aban (Novemba 4) ni zaidi ya tukio la kihistoria, ni ishara ya mwamko wa kisiasa, kufichua sura halisi ya ubeberu wa kimataifa na umoja wa kitaifa dhidi ya uingiliaji wa kigeni. Siku hii ni ukumbusho wa ukweli kwamba, uhuru, utu na usalama wa taifa vitahifadhiwa tu kupitia kusimama kidete, ufahamu na umoja wa watu dhidi ya satwa na kujitanua.

Kwa kusoma tena tukio hili, kizazi kipya cha leo kinaweza kuendeleza njia ya muqawama, utambuzi, na kudumisha mamlaka ya kujitawa, na kufanya mambo kwa uangalifu na kuwa macho dhidi ya ushawishi na uingiliaji wowote wa kigeni. Kutekwa Pango la Ujasusi (uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran) kulikuwa ni jibu la kujihami dhidi ya njama kubwa ya kukkabiliana na harakati ya Kiislamu ya watu wa Iran. Hatua hii iliuonyesha ulimwengu utambulisho huru na wa kupinga ubeberu wa Mapinduzi ya Kiislamu; utambulisho ambao uliiwezesha Iran, katika vita vya Juni mwaka huu (2025) kukabiliana peke yake na kutegemea nguvu zake za ndani, sio tu dhidi ya utawala wa Kizayuni bali pia dhidi ya mfumo mzima wa ubeberu kwa muda wa siku 12, na kuzuia maadui kufikia malengo yao. 3495268/

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: 13 aban ubalozi marekani
captcha