IQNA

14:30 - March 02, 2020
News ID: 3472521
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 7 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya wanafunzi ya Waislamu yameakhirishwa.

Sayyed Mohammad Javad Shooshtari, mkuu wa Akademia ya Harakati za Qur’ani ya Iran ambayo huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya wanafunzi Waislamu duniani amezungumza na IQNA na kusema mashindano hayo ambayo hufanyika mara moja kila miaka miwili yaliyokuwa wamepangwa kufanyika katika kipindi cha miezi michache ijayo.  Hatahivyo kutokana na kuibuka kirusi cha Corona na kutojulikana hatima ya kirusi hicho, mashindano hayo yameakhirishwa.

Akiashiria historia ya mashindano hayo, amesema Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) imekuwa ikiyafadhili mashindano ya Qur’ani ya wanafunzi Waislamu baada ya kila miaka miwili tokea mwaka 2006 kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano baina ya wanafunzi Waislamu kote duniani sambamba na kustawisha kiwango cha harakati za Qur’ani katika vyuo vikuu.

Amesema mashindano hayo ambayo hadi sasa yamefanyika katika mikoa ya Isfahan, Azarbaijan Mashariki, Khorassan Razavi na Tehran nchini Iran yamepokewa vizuri na wanafunzi wa vyuo vikuu kote duniani.  Shooshtari amesema tarehe ya mashindano yajayo itatangazwa baadaye.

Mripuko wa kirusi cha corona ulianzia katika mji wa Wuhan ulioko katika mkoa wa Hubei nchini China Desemba mwaka uliopita wa 2019.

Mbali na mikoa 30 ya China, hivi sasa kirusi hicho kimeshaenea kwenye zaidi ya nchi zisizopungua 60 duniani.

3470803

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: