IQNA

Mijumuiko ya kidini, mahafali za Qur’ani marufuku Nigeria katika Mwezi wa Ramadhani

10:28 - April 26, 2020
Habari ID: 3472704
TEHRAN (IQNA) – Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu Nigeria (NSCIA) limetangaza marufuku ya mijimuiko yote ya kidini katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mwenyekiti wa baraza hilo Sheikh Saad Abubakr amesema mijimuiko hiyo inajumuisha mahafali za kusoma na tafsiri ya Qur’ani Tukufu, Itikafu na sala ya Tarawih. Amesema Waislamu wote duniani wanapaswa kuchukua hatua sawa na hiyo ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona au COVID-19. Sheikh Saad Abubakr amesema Uislamu hauruhusu mtu kuhatarisha maisha yaw engine wakati wa kutekeleza ibada.

Hadi kufikia Aprili 25, watu 1,095 walikuwa wameambukizwa corona nchini Nigeria na miongoni mwao 32 wamefariki na wengine 208 wamepata afueni.

3893969

captcha