IQNA

15:28 - April 21, 2020
Habari ID: 3472688

Aliyeswalisha Ijumaa kwa siri Nigeria akamatwa

TEHRAN (IQNA) –Mhubiri wa Kiislamu Nigeria amekamatwa katika jimbo la Kano kaskazini mwa nchi hiyo baada ya kuswalisha Sala ya Ijumaa kwa siri kinyume cha amri ya serikali.

Aliyeswalisha Ijumaa kwa siri Nigeria akamatwa

Kwa mujibu wa taarifa, Gavana wa Jimbo la Kano Abdullah Gandujeh amesema imamu huyo alikiuka amri ya serikali ya kusitisha kwa muda swala za jamaa ili kuzuia kuenea corona au COVID-19.

Gavana hiyo amesema mijimuiko yote, ikiwemo ya kidini, imepigwa marufuku wakati wa kipindi hiki cha ugonjwa wa COVID-19.

Hadi kufikia Aprili 21, watu 665 walikuwa wameambukizwa corona Nigeria  huku 22 miongoni mwao wakipoteza maisha.

3893092

captcha