IQNA

Vituo 200 vya Qur’ani Jordan kuandaa darasa tahfidh

23:04 - July 27, 2020
Habari ID: 3473006
TEHRAN (IQNA)- Vituo 200 vya Qur’ani Tukufu nchini Jordan vimetangaza kuandaa darsa maalumu za kuhifadhi Qu’rani Tukufu kwa kuzingatia kanuni za afya wakati huu wa janga la corona.

Kwa mujibu wa televisheni ya Roya News, masomo hayo ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu yatafanyika mwaka huu lakini kwa idadi ndogo ya wanafunzi. Aidha kanuni zote za kiafya kuhusu ugonjwa wa corona zitazingatiwa.

Wanafunzi watajifunza kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu, maadili ya Kiislamu na hadithi za Mtume Muhammad SAW.

Tokea Machi 20, Jordan ilitangaza sheria ya kafyu ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Hadi sasa watu 1,168 wameambukizwa corona nchini Jordan na miongoni mwao 11 wamefariki dunia.

3912611

 

Kishikizo: jordan ، waislamu ، qurani ، tahfidh ، corona
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha