IQNA

Darul Iftaa ya Jordan

Ni haramu kwa wanaougua corona kushiriki swala za jamaa, ni haramu pia kuficha ugonjwa

12:42 - July 05, 2020
Habari ID: 3472932
TEHRAN (IQNA) – Darul Iftaa ya Jordan imetoa fatwa inayowapiga marufuku wagonjwa wa COVID-19 au corona kushiriki katika swala za jamaa.

Kwa mujibu wa tovuti ya arabic.rt, Fatwa hiyo imesema ni haramu kwa wagonjwa wa COVID-19 au wanaoshukiwa kuwa wameambukizwa ugonjwa huo kushiriki katika swala za jamaa.

Fatwa hiyo imetolewa kufuatia swali ambalo limeulizwa kuhusu kushiriki katika swala za jamaa, ikiwemo swala ya Ijumaa, wakati wa janga la COVID-19.

Halikadhalika fatwa hiyo imesisitiza kuwa ni haramu kwa Mwislamu kuficha au kutotoa taarifa iwapo ameugua ugonjwa wa COVID-19  na kwamba ni wajibu kwa wote kufungamana na maagizo ya kiafya ya kuzuia kuenea ugonjwa huo.

Hadi sasa watu miloni 11.2 wameambukziwa COVID-19 duniani huku wengine zaidi ya nusu milioni wakiwa wamepoteza maisha. Uongjwa huo wa kuambukiza unazidi kuenea kwa kasi kote duniani.

3908670

Kishikizo: jordan ، swala ، darul iftaa ، COVID-19
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha