IQNA

Swala ya Ijumaa yaanza tena nchini Jordan

22:35 - November 19, 2020
Habari ID: 3473374
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu Jordan amesema marufuku ya Swala ya Ijumaa nchini humo sasa imeondolewa.

Sheikh Mohammad Khalaileh amesema katika taarifa siku ya Alhamisi kuwa Swala ya Ijumaa itaswaliwa kote nchini humo wiki hii.

Amesisitiza kuhusu umuhimu kwa waumini kuzingatia kanuni za kiafya ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kutumia zulia au mkeka binafsi wa kuswalia na kutokaribiana wakati wa swala ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Misikiti ilifungwa Jordan mwezi Aprili kufuatia kuenea ugonjwa wa corona. Misikiti ilifunguliwa tena kwa swala za jamaa mwezi Juni na sasa swala ya Ijumaa itaruhusiwa kuanzia wiki hii.

Tokea ugonjwa wa corona uripotiwa mapema mwezi Machi hadi sasa, watu 169,000 wameabukizwa ugonjwa huo nchini Jordan ambapo watu 2,053 wamepoteza maisha.

 3936184

Kishikizo: jordan ، corona ، swala ya ijumaa
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha