IQNA

Al Azhar yazindua kampeni ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu

14:02 - September 01, 2020
Habari ID: 3473126
TEHRAN (IQNA) – Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri kimeanzisha kampeni maalumu ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia).

Kampeni hiyo inayojulikana kama “Uislamu Wasioujua’ imezinduliwa na Idara ya Utafiti wa Kiislamu ya Al Azhar katika mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook baada ya Qur’ani Tukufu kuvunjiwa heshima hivi karibuni barani Ulaya katika nchi za Sweden na Norway.

Afisa mwandamizi wa Al Azhar Bw. Nazir Ayad  amesema kampeni hiyo inalenga kuwasilisha taswira sahihi ya Uislamu miongoni mwa wale wenye chuki dhidi ya dini hii tukufu. Ayad ameongeza kuwa, taswira potovu kuhusu Uislamu imepelekea kuenea chuki dhidi ya Uislamu pamoja na matukufu yake.

Siku ya Ijumaa, wazungu wenye misimamo mikali ya kibaguzi waliteketeza moto nakala ya Qur’ani Tukufu katika mji wa Malmo nchini Sweden. Siku moja baada ya kitendo hicho kiliandaliwa maandamano dhidi ya Uislamu katika mji mkuu wa Norway, Oslo, ambayo yaliandaliwa na kundi linalojiita ‘Zuia Uislamu Norway’ (SION) ambapo washiriki walichanachana kurasa za Qur’ani Tukufu na kuzitemea mate. Vitendo hivyo vya kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu vinaendelea kulaani kote duniani.

3920273

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :