IQNA

Sweden yamzuia mwanasiasa kufika tukio la kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu, ghasia zaibuka

14:45 - August 29, 2020
Habari ID: 3473115
TEHRAN (IQNA) – Maandamano makubwa yameibuka kusini mwa Sweden Ijumaa usiku baada ya mwanasiasa wa Denmark anayepinga Uislamu kuzuiwa kuhudhuria hafla ya kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu.

Taarifa zinasema karibu watu 300 wenye chuki dhidi ya Uislamu walimiminika katika mitaa ya mji wa Malmo na kukabiliana na polisi.

Maandamano hayo yalijiri masaa machache baada ya waandamanaji kuteketeza nakala ya Qur’ani Tukufu, amesema msemaji wa polisi Rickard Lundqvist.

Rasmus Paludan, ambaye anaongoza chama cha chenye misimamo mikali cha mrengo wa kulia ambacho kinapinga Waislamu, alikuwa amepanga kufika Malmo kuhutubu katika mjumuiko huo wa kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu.

3472405

captcha