IQNA

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria yataka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru

20:05 - September 13, 2020
Habari ID: 3473164
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetoa wito wa kuachiliwa huru kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky pamoja na mkewe Malama Zinat Ibrahim ambao hali zao za kiafya zinazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.

Katika taarifa,

Jukwaa la Kielimu ambalo ni tawi la Harakati ya Kiislamu ya Nigeria limeeleza wasiwasi mkkubwa lilionao kwa afya ya Sheikh Zakzaky na mkewe wanaoshikiliwa gerezani na kutaka wawili hao waachiliwe huru na bila masharti yoyote.

Kundi hilo limesema kuwa, taarifa walizonazo zinaonyesha kuwa, hali ya kiafya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky pamoja na mkewe ni mbaya mno.

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe Malama Zeenat walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia Hussainia ya Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria. Waislamu wasiopungua 1,000, wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi katika shambulio hilo.

Mahakama Kuu ya Nigeria iliwahi kutoa hukumu iliyosisitiza kuwa Sheikh Ibrahim Zakzaky pamoja na mkewe hawana hatia yoyote na ikaamuru waachiliwe huru, lakini wawili hao wangali wanaendelea kuwekwa jela na hivi sasa hali zao za afya ni mbaya sana

Wakati huo huo, hatua kandamizi na za kikatili za polisi na jeshi la Nigeria dhidi ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky zingali zinaendelea na hadi sasa idadi kubwa ya wafuasi wa kiongozi huyo wa kidini wamewekwa kizuizini au wameuawa shahidi. Aidha vyombo vya usalama vimekuwa vikifanya kkila viwezalo kukwanmisha shughuli za kidini za Waislamu wa Kishia nchini Nigeria.

3472542

captcha