IQNA

Mawakili wa Sheikh Zakzaky wa Nigeria wataka aachiliwe huru

20:29 - July 18, 2020
Habari ID: 3472976
TEHRAN (IQNA) – Mawakili wa Sheikh Ibrahim Zakzaky wameitaka Mahakama Kuu ya Nigeria kutupilia mbali kesi dhdi ya yake itoe amri ya kuachiliwa huru mara moja mwanazuoni huyo na mke wake.

Mawakili wa kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria waliwasilisha pendekezo katika Mahakama Kuu ya Nigeria wakitaka tuhuma zote dhidi yake na mke wake zifutwe.

Masoud Shajareh, mkuu wa Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu amesema mwaka 2016 Mahakama Kuu ya Nigeria iliamuru Sheikh Zakzaky aachiliwe huru na alipwe fidia lakini serikali imekaidi amri hiyo.

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe Malama Zeenat walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia Hussainia ya Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria. Waislamu wasiopungua 1,000, wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi katika shambulio hilo.

Hatua kandamizi na za kikatili za polisi na jeshi la Nigeria dhidi ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky zingali zinaendelea na hadi sasa idadi kubwa ya wafuasi wa kiongozi huyo wa kidini wamewekwa kizuizini au wameuawa shahidi.

3472030/

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha