IQNA

IHRC yaitaka Nigeria imuachilie huru Sheikh Zakzaky na mke wake

21:31 - July 29, 2020
Habari ID: 3473012
TEHRAN (IQNA) –Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu (IHRC) yenye makao yake London, Uingereza imeitaka serikali ya nchi hiyo imuachilie huru mara moja mwanazuoni wa Kiislamu nchini humo, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake ambao wamekuwa wakishikiliwa kizuizini tokea mwaka 2015 kwa mashtaka yasiyo na msingi.

IHRC imemuandikia barua Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ikimtaka amuachilie huru Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake, Bi. Mallima Zeenah.

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe Malama Zeenat walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia Hussainia ya Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria. Waislamu wasiopungua 1,000, wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi katika shambulio hilo.

Hatua kandamizi na za kikatili za polisi na jeshi la Nigeria dhidi ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky zingali zinaendelea na hadi sasa idadi kubwa ya wafuasi wa kiongozi huyo wa kidini wamewekwa kizuizini au wameuawa shahidi.

Barua aliyoandikiwa Buhari na IHRC pia  inamkumbusha kuhusu mauaji ya Zaria ambayo sasa yanachunguzwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC.

34721310

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha