IQNA

10:45 - August 13, 2020
News ID: 3473062
TEHRAN (IQNA) – Wafuasi wa kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Abuja wakitaka serikali imuachilie huru.

Katika maandamano hayo ya Jumatano, waandamanaji wao waliokuwa wakiandamana kwa amani wameitaka serikali ya Nigeria imuachilie huru Sheikh Zakzaky na mke wake.

Aidha wamesema kuendelea kushikiliwa korokoroni Sheikh Zakzaky na mke wake ni kinyume cha sheria na kuongeza kuwa wanapaswa kuachiliwa huru bila masharti.

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe Malama Zeenat walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia Hussainia ya Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria. Waislamu wasiopungua 1,000, wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi katika shambulio hilo.

Hatua kandamizi na za kikatili za polisi na jeshi la Nigeria dhidi ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky zingali zinaendelea na hadi sasa idadi kubwa ya wafuasi wa kiongozi huyo wa kidini wamewekwa kizuizini au wameuawa shahidi.

Maandamano ya kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru hufanyika mara kwa mara nchini humo.

تظاهرات هواداران شیخ زکزاکی در پایتخت نیجریه
 
تظاهرات هواداران شیخ زکزاکی در پایتخت نیجریه
 
تظاهرات هواداران شیخ زکزاکی در پایتخت نیجریه 

3916331

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: