IQNA

Waalimu watano wa Qur'ani wauawa katika hujuma Somalia

22:16 - September 18, 2020
Habari ID: 3473182
TEHRAN (IQNA) – Waalimu watano wa Qur'ani wameuawa baada ya kufyatuliwa risasi na magadi katika kikao cha kusoma Qur'ani Tukufu kusini mwa Somalia.

Hujuma hiyo ya kusikitisha imejiri Alhamisi asubuhi katika mji wa Rage Ele, katika eneo  la Middle Shabelle. Mkuu wa Wilaya ya Adale katika eneo hilo amesema mauaji ya raia wasio na hatia wakiwemo waalimu wa dini ni jambo lisilokubalika.

Ameongeza kuwa, taarifa za awali zimebaini kuwa hujuma hiyo ilikuwa ni shambulio la ulipizaji kisasi. Amefafanua kwa kusema kuwa waalimu waliouawa na washambuliaji walikuwa ni kutoka koo tafauti na kwamba magaidi waliotekeleza hujuma hiyo walikuwa wanalipiza kisasi.

Afisa mwandamizi wa polisi mjini Jowhar, mji mkuu wa Middle Shabele, Ali Nour Hassan amesema wahubiri kadhaa wa Kiislamu walijeruhiwa katika tukio hilo na wanapata matibabai katika Hospitali ya Jowhar.

Ameongeza kuwa wakuu wa eneo hilo wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

3472594

Kishikizo: somalia ، magaidi ، waalimu ، qurani tukufu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :