IQNA

Spika ya Bunge la Iran

Utiwaji saini mapatano baina ya China na Iran ni indhari muhimu kwa Marekani

15:36 - April 04, 2021
Habari ID: 3473781
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema kutiwa saini mapatano ya ushirkiano wa Iran na China ni onyo muhimu kwa Marekani na kuongeza kuwa, matukio ya kimataifa yanachukua mkondo wa kasi ambao ni kwa hasara ya Marekani.

Akizungumza katika kikao cha leo bungeni, Mohammad Baqer Qalibaf, Spika wa Bunge la Iran ameongeza kuwa: "Kwa bahati nzuri sheria ya kistratijia kuhusu kuondolewa vikwazo imepitishwa, sekta ya nyuklia imeanza mkondo mpya wa kazi na hivi sasa hali inabadilika na kuwa kwa maslahi ya Iran." Amesema siku za nyuma vikwazo vilienda sambamba na kusitishwa shughuli za nyuklia za Iran lakini sasa kuna vikwazo lakini sekta ya nyukklia ya Iran inastawi na upande wa pili unapata hasara ukiendelea kuchelewesha mambo.

Qalibaf amesema mafanikio ambayo Iran imeyapata katika uga wa diplomasia kivitendo yatapelekea kuondolewa vikwazo kikamilifu na hivyo taifa la Iran litapata manufaa ya kiuchumi.

Spika wa Bunge la Iran amesisitiza kuwa, Wamarekani wanapaswa kuondoa vikwazo vyote dhidi ya Iran kivitendo kwani kutoa ahadi kwenye makaratasi tu si jibu sahihi kwa watu wa Iran.

Qalibaf amesema mapatano ya kistratijia ya miaka 25 yaliyotiwa saini karibuni baina ya Iran na China ni onyo muhimu kwa Marekani. Amesema mapatano hayo ni ujumbe kwa Marekani kuwa matukio ya kimataifa sasa yanachukua mkondo ambao ni hasara kwake. Amesema Marekani haina uwezo wa kuchukua maamuzu ya upande mmoja kuyalazimisha mataifa mengine yafanye inavyotaka.

Hati ya  ushirikiano wa pande zote kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Watu wa China kwa jina la "Mpango wa Miaka 25" ilisainiwa Jumamosi iliyopita hapa Tehran na Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na mwenzake wa China Wang Yi. 

3962322

Kishikizo: Qalibaf iran marekani china
captcha