Nchi zilizotangaza leo kuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni pamoja na Malaysia, Indonesia, Australia, Japan na baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi. Katika nchi hizo Waislamu wameshiriki katika Sala ya Tarawih kwa kuzingatia kanuni za kiafya za kuzuia kuenea COVID-19.
Nchi zingine kama vile Iraq, Iran, Tanzania na Kenya zimetangaza rasmi kuwa Aprili 14 ni siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.