IQNA

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Misri Wasoma Qur’ani kwa Sauti ya Pamoja + Video

12:44 - December 25, 2025
Habari ID: 3481714
IQNA – Wachezaji wa timu ya taifa ya kandanda ya Misri wamesoma aya za Qur’ani Tukufu kwa sauti ya pamoja kabla ya mechi dhidi ya Zimbabwe katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Klipu ya video imetolewa ikionyesha wachezaji wa Misri wakisoma Qur’ani ndani ya chumba cha kubadilishia nguo kabla ya kuanza mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika uliofanyika Morocco, kama ilivyoripotiwa na gazeti la Yeni Shafak.

Usomaji huo wa pamoja wa Qur’ani na wachezaji wa Misri umeenea sana na kupata ufuatiliaji mpana. Katika video hiyo, walisoma Surat al-Fātiha mara moja na Surat al-Ikhlās mara tatu, wakitafuta baraka na ushindi kabla ya kuingia uwanjani.

Katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Misri ilikabiliana na Zimbabwe na kufanikiwa kushinda kwa mabao 2–1.

Misri ni taifa la Kaskazini mwa Afrika lenye idadi ya watu takribani milioni 100. Takriban asilimia 90 ya raia wake ni Waislamu. Shughuli za Qur’ani ni jambo la kawaida katika nchi hii yenye Waislamu wengi, na historia ya ulimwengu wa Kiislamu imejaa makari mashuhuri wa Qur’ani waliotoka Misri, wa zamani na wa sasa.

4324777

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu soka misri
captcha