IQNA

Hujjatul-Islam Panahian: Dini Ndiyo Nguvu Kuu Inayounda Mabadiliko ya Dunia

16:06 - November 27, 2025
Habari ID: 3481577
IQNA – Mwanazuoni wa Chuo Kikii cha Dini (Hawzah) cha Qom, Hujjatul-Islam Alireza Panahian, ameeleza kuwa dini ndiyo nguvu kubwa zaidi miongoni mwa sababu zinazounda mabadiliko ya kimataifa.

Akihutubia mkutano wa kielimu katika Haram ya Hadhrat Masoumah (SA) jijini Qom, alisema jamii ya Kiislamu lazima iimarike katika uelewa sahihi wa dini, ikabiliane na upotoshaji, na iondoe udhaifu katika nyanja kama uchumi na mahusiano ya kijamii ili iweze kuchukua nafasi yenye nguvu zaidi katika mabadiliko ya dunia.

Hujjatul-Islam Panahian amesisitiza kuwa dini daima imekuwa miongoni mwa nguvu kuu zinazoathiri maisha ya binadamu. Aliongeza kuwa mwenendo wa miongo ya hivi karibuni unaonyesha kuwa wazo la kuondoa dini katika uwanja wa kijamii na kisiasa ni kosa, kwani hata harakati nyingi zenye ushawishi duniani leo, hata zile zinazopinga dini, zinajipatia nguvu kutoka katika itikadi za kidini au zile zinazofanana na dini.

Akitaja Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kama mfano mashuhuri wa nguvu ya dini katika enzi ya kisasa, alisema harakati hiyo ya kidini iliathiri siasa za kikanda na kimataifa, na leo hii mapambano ya Kiislamu ni kielelezo cha nguvu hiyo.

Akirejelea maendeleo ya Iran katika ulinzi na nyanja nyingine, Panahian alisema: “Wataalamu na wanasayansi wetu vijana wengi wameingia katika uwanja wa teknolojia kwa msukumo wa kidini na roho ya mapambano, na wamepata mafanikio makubwa ya kimkakati.”

Aliongeza kuwa kipimo muhimu cha kutambua dini ya kweli ni uwezo wa kuunda nguvu ndani ya mtu binafsi na jamii. “Aina yoyote ya dini inayosababisha udhaifu, ulegevu au kujitenga ni dalili ya upotoshaji.”

Hujjatul-Islam Panahian pia alisisitiza jukumu la kijamii la misikiti, akisema misikiti lazima iwaandae waumini wenye nguvu na kuimarisha mazingira ya mawasiliano na ushirikiano kati ya waumini. “Msikiti ambao ni mahali pa kupita tu kwa sala umepoteza jukumu lake halisi,” alisema.

 4319295

Kishikizo: jamii dunia dini kiislamu
captcha