IQNA

19:13 - April 21, 2021
News ID: 3473836
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Ujerumani imeidhinisha adhana kupitia vipaza sauti misikitini katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kote katika nchi hiyo.

Waislamu nchini Ujerumani wamebainisha furaha yao kupitia uamuzi huo. Serikali ya kifiderali Ujerumani inasema kuruhusu adhana kwa vipaza sauti misiktini ni hatua ya kuwaunga mkono Waislamu wakati huu wa janga la COVID-19.

Mwaka jana pia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, misikiti 100 Ujerumani na Uholanzi ilipata idhini ya kuadhini kupitia vipaza sauti.

Kwa ujumla adhana misikiti kupitia vipaza sauti ni marufuku Ujerumani isipokuwa tu wakati wa minasaba maalumu.

Waislamu Ujerumani wanasema ni haki yao kusikia adhana kwa vipaza sauti misikitini lakini aghalabu ya miji ya Ujerumani hairuhusu adhana.

Hivi sasa wakati wengi hawawezi kutoka majumbani kutokana na janga la COVID-19, Waislamu wengi wanasema kuna umuhimu zaidi kusikia sauti ya adhana.

3966131

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: