IQNA

Ufalme Saudia waweka vizuizi katika adhana misikitini

20:28 - May 24, 2021
Habari ID: 3473943
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Masuala ya Kiislamu katika Ufalme wa Saudi Arabia imetangaza kuweka vizuizi katika utumizi wa vipaza sauti misikitini nchini humo.

Kwa mujibu wa amri iliyotolewa na Abdul Latif Al Sheikh, Waziri wa Masuala ya Kiislamu Saudia kwa misikiti yote katika ufalme huo, vipaza sauti vitatumika tu wakati wa adhana na iqama na pia sauti  inapaswa kuwa kiwango cha chini zaidi iliyvyo hivi sasa.

Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News, amri hiyo imetolewa kwa mujibu wa fatwa za wanazuoni maarufu Sheikh Mohammed bin Saleh Al Othaimeen and Saleh Al Fawzan ambao wanasema vipaza sauti vinapaswa kutumika tu wakati wa adhana na iqama.

/3474793

Kishikizo: saudia adhana
captcha