IQNA

Idhaa ya Qur'ani Misri kurusha hewani qiraa nadra

18:13 - August 24, 2021
Habari ID: 3474222
TEHRAN (IQNA) - Mkurugenzi mpya wa Idhaa ya Qur'ani ya Radio ya Misri alisema programu maalum itarushwa na idhaa hiyo siku za usoni ambayo inaangazia qiraa nadra za Qur'ani ambazo ni za wasomaji Wamisri.

Ridha Abdulsalam ndiye mtu wa kwanza ambaye, licha ya ulemavu mikononi mwake, ameteuliwa kama mkurugenzi wa Idhaa ya Qur'ani nchini Misri.

Alichaguliwa kuwa mtangazaji bora wa Idhaa ya Quran na baadaye akatajwa kama mkurugenzi wa idhaa hiyo kutokana na sifa alizopata katika kipindi cha miaka 30 ya kufanya kazi katika vipindi tofauti vya radio.

Abdulsalam amesema kuwa atajaribu kuhakikisha kuwa vipindi vipya vinarushwa na kituo na kwamba atauliza wataalam wakuu katika sayansi ya kijamii ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar na watu wengine wa masomo nchini kumsaidia katika suala hili.

Aliongeza kuwa kituo hicho pia kitatumia wasomi katika mipango yake kufafanua fikra za Kiisilamu kwani Uislamu ni dini kamili inayopaswa kuarifishwa kwa watu wote duniani.

Alisema idhaa hiyo inasambaza Uislamu wa wastani  kama ulivyofundishwa naa Mtukufu Mtume Muhammad SAW,  ambao hauhusiani na misimamo mikali na ugaidi.

Alisema zaidi kuwa kurusha hewani qiraa  nadra za Quran ambazo hazijarushwa na kituo hadi sasa, ni miongoni mwa mipango yake mingine.

Alisema kuwa qiraa ya Qur'ani Tukufu itachukua asilimia 80 ya vipindi vya idhaa hiyo.

3992275

captcha