IQNA

Qarii wa Misri afariki akiwa na umri wa miaka 26

21:44 - September 15, 2021
Habari ID: 3474299
TEHRAN (IQNA)- Qarii na hafidh wa Qur’ani Tukufu Misri, Mahmoud Abdul Sattar al Utwa amefariki akiwa na umri wa miaka 26.

Kwa mujibu wa taarifa, qarii huyo kijana amefariki kufuatia mshtuko wa moyo.

Qarii Mahmoud alikuwa ni  mwenyeji wa kijiji cha Shabana katika jimbo la Sharqia la nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Baba yake anasema Mahmoud alihifadhi Qur’ani Tukufu utotoni. Kutokana na sauti yake nzuri alianza kujifunza qiraa ya Qur’ani Tukufu kutoka kwa wasomi bingwa nchini humo.

Mwendazake alikuwa anajishughulisha Zaidi katika qiraa ya Qur’ani na kwafunza Qur’ani watoto na vijana kijini kwake na vijiji vya karibu.

Misri ni nchi ambayo imepata umashuhuri duniani kutokana na idadi kubwa ya wasomaji Qur’ani hasa wale wenye vipaji vya kipekee.

3997655

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha