IQNA

Majaji wa tamasha la Iran la qiraa ya Qur’ani kwa kuiga watangazwa

20:44 - February 22, 2025
Habari ID: 3480253
IQNA – Hatua ya mwisho ya toleo la pili la Tamasha la Usomaji wa Qur'ani kwa kuiga inaanza leo huko Qazvin, Iran, na waandaaji wametangaza majina ya wajumbe wa jopo la majaji.

Jopo hilo linajumuisha wataalamu 14 wakuu wa Qur'ani nchini, wakihudumu kama majaji, washauri na wasimamizi.

Majaji ni pamoja na Gholam Reza Shahmiveh, Mohammad Kazem Naddaf, Ahmad Moqimi, Vahid Nazarian, Qassem Moqaddami, Hamed Valizadeh, Ali Akbar Kazemi na Seyed Mohammad Hadi Qassemi.

Wakati huo huo, Mohammad Purashuri, Mojtaba Mohammadbeigi, Hadi Rahimi, Amin Rahimi, na Mehdi Rashtbari wanahudumu kama wasimamizi  na Ali Reza Lotfi anawasaidia washindani kama mshauri.

Akizungumza na IQNA, Hujjatul Islam Seyed Mostafa Majidi, Mkurugenzi Mkuu wa Mambo ya Wakfu na Hisani katikak Mkoa wa Qazvin, amesema kwamba mashindano hayo yanafanyika katika makundi matatu ya umri wa miaka 9-13, 13-16, na 16-20.

Kwa mujibu wa Majidi, zaidi ya vijana 3,000 wenye shauku ya Qur’ani walituma usomaji wao mtandaoni baada ya kutangazwa kwa tamasha hilo. Alieleza kuwa “Baada ya mchujo wa awamu tatu, majaji walichagua washiriki 50 wa fainali, ambao watakusanyika Qazvin kwa mashindano.”

Ratiba ya mashindano inaonyesha kuwa mashindano yameanza jioni ya Februari 22 na yataendelea hadi Februari 24 na hafla ya kufunga ikifanyika Februari 25.

Majidi alieleza kuwa, mbali na tukio kuu, kutakuwa na mikusanyiko ya Qur’ani inayohusisha Qari wa kimataifa na wa ndani katika mkoa mzima wa Qazvin. “Tumepanga vikao 22 vya Qur’ani ili kuboresha mazingira ya tamasha, pamoja na maonyesho ya bidhaa za Qur’ani na utamaduni katika eneo la Imamzadeh Hossein.”

Tamasha la mwaka huu linajengwa juu ya mafanikio ya tukio la kwanza, ambalo lilianzisha dhana ya usomaji wa kuiga – ambapo washiriki huiga mitindo ya wasomaji mashuhuri wa Qur’ani – kwa hadhira pana zaidi.

Tamasha la mwaka jana lilifanyika katika Imamzadeh Saleh, Tehran, mnamo Mei.

3491958

captcha