IQNA

Wanawake katika Uislamu

Hajar Sa’eddin; Mwanamke wa kwanza kuwa mkurugenzi wa Idhaa ya Qur'ani ya Misri

12:54 - February 16, 2023
Habari ID: 3476569
TEHRAN (IQNA) – Hajar Sa’eddin aliongoza Idhaa ya Qur’ani ya Misri kwa muda wa miezi 7. Alikuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.

Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar, Hajar aliteuliwa kushika wadhifa huo mwaka wa 1997 baada ya Abdul Samad al-Dasoughi kustaafu kama mkurugenzi wa redio hiyo.

Kabla ya hapo, alikuwa akitayarisha kipindi kiitwacho "Dini na Maisha", ambacho kilikuwa na tafsiri ya aya za Qur'ani kwa mtazamo wa dini na sayansi. Pia aliwahi kuwa naibu mkuu wa idhaa hiyo.

Kipindi hicho kilirushwa na Idhaa ya Qur'ani ya Misri katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuvutia idadi kubwa ya wasikilizaji.

Hajar anasema yeye sio mwanamke wa kwanza kufanya kazi kama mtangazaji katika Idhaa ya Qur'ani akiongeza kuwa kabla yake, Fatima Taher alikuwa mtangazaji wa redio katika kituo hicho cha redio mnamo 1979.

Hapo awali, anabainisha, kulikuwa na marufuku ya kutangaza sauti ya wanawake kwenye Redio ya Qur'ani ya Misri.

Leo, kuna wanawake wengi wanaofanya kazi kwenye redio hii katika nyadhifa tofauti, anadokeza.

Akirejelea historia ya Idhaa ya Qur'ani ya Misri, Hajar anasema ilianzishwa Machi 1964 kwa amri ya rais wa wakati huo wa Misri Gamal Abdel Nasser.

Visomo vya kwanza vya Qur'ani vilivyotangazwa kwenye redio vilikusanywa na Sheikh al-Husari, anasema, akiongeza kwamba Maustadh kama vile Abdul Basit Abdul Samad na Mahmoud Ali al-Bana waliendelea na njia yake.

Hajar Sa’deddin; First Woman Who Headed Egypt’s Quran Radio

Hajar aliteuliwa kuwa balozi wa amani wa Umoja wa Mataifa mwaka 1996 kwa jukumu lake katika kuinua nafasi ya wanawake katika ulimwengu wa Kiarabu.

4122126

captcha