IQNA

Ufaransa yaendelea kufunga misikiti

11:48 - October 28, 2021
Habari ID: 3474484
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa imetangaza mpango wa kufunga misikiti kadhaa na pia kufuta vibali vya jumuiya kadhaa za Kiislamu kwa kisingzio cha kuzuia kuenea misimamo mikali.

Baada ya kufunga msikiti katika mji wa Allones kwa muda wa miezi sita, Waziri wa Mambo ya Ndani Ufaransa Gerald Darmanin amedia kuwa, hotuba katika msikiti huo zinachochea chuki dhidi ya Ufaransa.

Ameongeza kuwa, jumuiya saba za Kiislamu ambazo zina majengo ya kuendeshea shughuli zao nazo pia zitafutiwa vibali ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Aidha amesema misikiti 92 kati ya 2,500 nchini humo imefungwa  na kwamba tokea Septemba 2020 vibali vya raia 36,000 wa kigeni navyo pia vimebatilishwa.

Katika miezi ya hivi karibuni wimbi la chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa limeshadidi ambapo Waislamu wengi wamekuwa waiandamwa kwa mashinikizo na vitendo vya bughuda ha na mauadhi na hata wakati mwingine matukufu ya dini yao kutusiwa na kuvunjiwa heshima.

Serikali ya Paris imepitisha  “Sheria ya Kuimarisha Thamani za Kijamhuri” ikidai kwamba, muswada huu haukinzani na dini nyingine na lengo lake hasa ni kutetea uhuru. Rais wa Ufaransa katika kutetea muswada huo amesema, unalenga kusaidia thamani za Ufaransa kama usawa wa kijinsia, usekurali na kung’oa mizizi ya fikra za kuchupa mipaka.

Hivi sasa Waislamu nchini Ufaransa wameingiwa na wasi wasi mkubwa kwani baada ya serikali kuanza kufunga misikiti sasa imegukia biashara zao.

Ufaransa ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, kuna zaidi ya Waislamu milioni 5.7 Ufaransa ambao ni takribani asilimia 8.8 ya watu wote nchini humo.

3476225

captcha