IQNA

Katibu Mkuu wa OPEC atembelea Haram Takatifu ya Imam Ali AS

17:21 - January 10, 2022
Habari ID: 3474789
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Shirika la Nchi Zinazoua Mafuta Kwa Wingi Duniani (OPEC) ametembelea Haram Takatifu ya Imam Ali AS mjini Najaf, Iraq.

Mohammed Sanusi Barkindo akiwa ameandamana na ujumbe ametembelea eneo hilo takatifu na amesisitiza kuhusu umuhimu wa hadhi ya mji mtakatifu wa Najaf katika ulimwengu wa Kiislamu.

Katika safari yake nchini Iraq, Barkindo amefanya mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu wa nchi hiyo mbali na kutembelea maeneo kadhaa ya kidini na kihistoria.

Barkindo ambaye ni mwanasiasa wa Nigeria alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa OPEC Juni mwaka 2016 na muda wake unamalizika mwaka baadaye mwaka huu.

زیارت رئیس سازمان اوپک از بارگاه مطهر امام علی (ع)

زیارت رئیس سازمان اوپک از بارگاه مطهر امام علی (ع)

زیارت رئیس سازمان اوپک از بارگاه مطهر امام علی (ع)

4027327

Kishikizo: barkindo ، imam ali as ، opec
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha