IQNA

Idul Fitr: Idi wanayostahiki waja wema

15:25 - May 02, 2022
Habari ID: 3475198
TEHRAN (IQNA)- Kinachowangoja waumini baada ya mfungo wa mwezi mmoja ni Idi adhimu ambayo imetolewa kwa wale ambao wametoka kwa mafanikio katika Ramadhani ambao ni mwezi wa ugeni na rehema zisizo na kikomo za Mwenyezi Mungu

Waislamu huadhimisha siku ya kwanza ya mwezi mwandamo wa Shawwal kama Idul Fitr; hii ni moja ya sikukuu kkubwa kwa Waislamu. Mwisho wa Ramadhani na kuanza kwa Shawwal hutangazwa baada ya kuona mwezi mwandamo. Kufunga ni haramu katika siku ya Idul Fitr.

Mtume Muhammad (SAW) anaashiria Idul Fitr katika hadithi, akisema: "Inapoanza siku ya Idul Fitr, Malaika hushuka duniani, ambapo husimama kwenye sehemu za barabara, wakiita kwa sauti inayosikika kwa viumbe vyote vya Mwenyezi Mungu, isipokuwa watu na Majini; 'Enyi Umma wa Muhammad (saw)! Njooni kwa Mola wenu Mlezi, Mtukufu na Mwingi wa Rehema, anaye kuruzuku, na anayesamehe madhambi makubwa.”

Waislamu wanatoa misaada kwa wasiojiweza kwa njia Zaka katika siku hii huku pia wakiwa wanasali sala ya Idul Fitr kwa jamaa..

Kugawa sehemu ya mali ya mtu kama Zakat al-Fitr inachukuliwa kuwa kitendo kinachostahiki na kinachosaidia kufunga. Ingawa thamani ya Zakat hii inaweza kuwa ndogo, inadhihirisha namna Waislamu wanavyowazingatia wale wanaohitaji na jaribio la waumini kukidhi mahitaji ya wanadamu wenzao katika jamii.

Kwa mujibu wa Imamu Sadiq (AS), aya ya 14 ya Sura Al-A’la isemayo “Mwenye kufanikiwa ni yule anayejitakasa” inahusu wale wanaotoa Zaka ya Fitri. Katika riwaya nyingine, Imam Sadiq (AS) anasema Mwenyezi Mungu atakubali funga ya mwenye kuimaliza kwa neno na kitendo sahihi, na kuongeza kuwa Zaka ya Fitri ni kitendo hicho kinachostahiki.

Zakat al-Fitr ni kilo tatu za chakula kikuu cha mtu na inaweza kuwa ngano, mchele, tende, shayiri, zabibu, au pesa yenye thamani ya kilo tatu.

Zaidi ya kutoa Zakat, Waislamu hukusanyika katika sala za jamaa asubuhi ya Idul Fitr. Wanasherehekea Idi wao kwa wao na kusherehekea pia katika jamii. Wanamshukuru Mungu kwa kuwapa nafasi ya kufunga na kumwomba Mungu awahifadhi mkabala wa maovu.

3478748

captcha