IQNA

15:41 - May 03, 2022
Habari ID: 3475201
TEHRAN (IQNA) Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamua ametuma salamu za mkono wa Idi kwa Waislamu na viongozi wa nchi za Kiislamu duniani kote

 

Katika ujumbe wake, Rais wa Iran amesema kuwadia siku kuu ya Idul Fitr ni dhihirisho la imani, na kustawi ucha Mungu sambamba na ubora wa mwanadamu.

Aidha rais wa Iran aimeitaja Idul Fitr kuwa siku kuu ya kunawiri maumbile ya mwandamu na matumaini ya waja wema kupata thawabu kutokana na amali zao njema kutoka kwa Mola Muumba. Rais wa Iran ameelezea matumaini yake kuwa, kwa mnasaba wa Idul Fitr Waislamu wataimarisha umoja na mshikamano wao ili waweze kufikia malengo matukufuya Uislamu na jambo hilo litapelekea kuhitimishwa migogoro na kupatikane amani na usalama zaidi.

Maelfu ya Waislamu wa Iran leo wameshiriki katika Sala ya Idul Fitr baada ya kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Baadhi ya mataifa ya Kiislamu kama Saudi Arabia, Uturuki, Misri, Qatar, Kuwait na Palestina yaliadhimisha sikukuu ya Idul Fitr jana huku mataifa mengine ya Kiislamu kama Iran, Tanzania, Pakistan na Iraq yakisherehekea sikukuu hiyo Jumanne ya leo.

Shirika la Habari la IQNA Linatoa mkono wa pongezi wa Idul Fitri kwa Waislamu kote duniani hususan wasomaji wa tovuti hii.

4054562

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: